Vijana wakiondoa mafuta yaliyomwagika barabarani.
Mwonekano wa eneo hilo.
Usafishaji wa barabara kwa maji ukiendelea.
Mfereji uliojaa mafuta yaliyomwangika.
Ilani inayowajulisha madereva utelezi uliokuwa mbele.
GARI lililokuwa na mafuta ya mawese jana usiku lilikwanguliwa na gari
jingine wakati limeegesha kando ya Barabara ya Nyerere eneo la
Vingunguti jijini Dar es Salaam na kusababisha kufunguka kwa loki za
matenki ya mafuta hayo na kuyafanya yamwagike katika eneo kubwa la
barabara karibu na kituo cha reli cha Tazara.
Tukio hilo lilisababisha utelezi katika barabara hiyo ambapo ungeweza kuleta ajali kwa magari yaliyokuwa yakipita eneo hilo.
Katika kukabili tatizo hilo wahusika
walihakikisha utelezi huo unaondolewa kwa kusafishwa kwa maji kama
kamera ya mtandao huu ilivyofika eneo hilo leo.
HABAR/PICHA: NA DENIS MTIMA/GPL

Note: Only a member of this blog may post a comment.