Friday, October 16, 2015

Anonymous

AJALI MBAYA MORO: Helikopta Imeanguka na Kulipuka…Waziri NYALANDU Amtaja Mbunge wa CCM Aliyekuwemo!

Usiku wa October 15 2015 zinatoka taarifa kupitia Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu kuhusu ajali ya helikopta iliyotokea kwenye mbuga ya wanyama ya Selous ikiaminika kuwa na Wanasiasa ndani yake.

Taarifa aliyoitoa imeeleza hivi >>> ‘Tumetuma vikosi vya maafisa na maaskari katika eneo la Selous kulikotokea ajali ya helikopta katika harakati za uokozi, ajali ya helikopta imetokea katika kitalu R3 ndani ya mbuga ya Selous na mashuhuda wanasema ilianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha‘
‘Mashuhuda wa ajali ya helikopta iliyotokea Selous walikuwa kitalu R2 na walishuhudia ikianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha Kitalu R3, Maafisa na Maaskari wanaelekea eneo la tukio kutokea Msolwa na Matambwe na tumeagiza vikosi vilivyo kwenye doria Selous kushiriki uokoaji‘

Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa (CCM)
‘Mashuhuda wa ajali ya helikopta Selous walikuwa Kitalu R2 wanasema ilianguka baada ya majira ya saa 12 jioni na kulipuka, serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii inachukua hatua zote kuwafikia wahanga na majeruhi wa ajali ya helikopta Selous usiku huu‘

‘Nimeagiza section 2 zenye askari 16 kutoka Matambwe na Msolwa (Selous) kwenda eneo la tukio, RPC Morogoro na mkuu kanda ya Msolwa (Selous) wanashirikiana, hatujui kitakachokuwa kimewapata wasafiri ndani ya helikopta iliyoanguka akiwepo Mh, Filikunjombe, tuungane kuwaombea kwa Mungu‘ <<< Lazaro Nyalandu

Hayo ndio maelezo aliyoyatoa Waziri Lazaro Nyalandu kupitia twitter page yake.
Hatujui kitakachokuwa kimewapata wasafiri ndani ya helikopta iliyoanguka, akiwepo Mh, Filikunjombe. Tuungane kuwaombea kwa Mungu.
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) October 15, 2015

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.