LIKIZO! Mkongwe wa sinema Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka kuwa
amelazimika kujipa likizo ya lazima kwa kutofanya shughuli za sanaa hadi
pale uchaguzi utakapopita.
Akizungumza
na mwandishi wetu hivi karibuni, JB alisema ameamua kusimama kazi zake
za sanaa kwani kwa sasa kila mtu anawaza mambo ya uchaguzi na hakuna
chochote anachoweza kufanya kikapokelewa bila ushabiki wa vyama.
“Nimeweka kila kitu pembeni mpaka uchaguzi huu umalizike maana kila
mtu yuko bize na mambo ya uchaguzi, huyu anasema hivi huyu anasema vile,
tumuombe tu Mungu atuvushe salama na mambo yetu yaendelee kama
kawaida,” alisema JB.
Note: Only a member of this blog may post a comment.