Friday, September 11, 2015

Anonymous

TFF Yampiga Stop Kocha YANGA SC

Mohammed Mdose, Dar es Salaam
KOCHA wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali, atalazimika kukosa mechi mbili za Ligi Kuu Bara kutokana na kuwa kwenye kozi ya makocha Leseni C inayotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kutokana na Pondamali kuhudhuria kozi hiyo ya wikiL mbili ambayo imeanza Jumanne ya wiki hii kwenye Ofisi za TFF, hatakuwa na timu yake kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union na Tanzania Prisons.

Hivi karibuni TFF ilitoa agizo kwa kila kocha wa ligi kuu kuwa hataruhusiwa kukaa kwenye benchi kama hana leseni ya ukocha kuanzia Leseni C, hivyo Pondamali amelazimika kuhudhuria ili baadaye asije kupata usumbufu.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Pondamali alisema kuwa kutokana na kozi hiyo, kwa muda wote huo wa wiki mbili amejiweka pembeni na timu hiyo mpaka kozi itakapomalizika, hivyo hata kwenye mechi za ligi hatakuwepo.

Alisema kuwa licha ya kutokuwepo kwenye benchi lakini mambo hayatakwenda kombo kwani kocha mkuu wa timu hiyo, Mdachi, Hans van Der Pluijm, naye ni mwalimu mzuri wa makipa, hivyo ataendelea kuwanoa bila wasiwasi.

“Sitakuwa na timu kwa wiki mbili, kwa hiyo mechi mbili za ligi nitazikosa, lakini hakuna kitakachoharibika kwa kuwa hata kocha Hans (Pluijm) naye ni kocha mzuri wa makipa, atakuwa nao.

“Nina vyeti kibao vya ukocha vingine nimevipata Brazil, lakini TFF waliposema hawavitambui wao wanataka kuanzia Leseni C na bahati nzuri kozi inafanyika hapa Dar, nikaona bora nije kuhudhuria ili nisije kupata shida baadaye,” alisema Pondamali.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.