Mohammed Mdose, Dar es Salaam
LICHA ya makocha wenzake
kuziandaa timu na kujua ubora wake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara,
hali ya mambo ni tofauti kwa Kocha Mkuu wa Majimaji, Mika Lonnstrom,
raia wa Finland, ambaye mpaka sasa hajajua uimara wa kikosi chake, hivyo
anataka kukijaribu kwenye mechi nne za mwanzo wa ligi.
Majimaji wataanza ligi kwenye uwanja wao
wa Majimaji Songea kwa kucheza na JKT Ruvu, kisha Kagera Sugar halafu
watawafuata Mgambo JKT, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, halafu Mtibwa Sugar
kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha
huyo aliyetua Majimaji miezi miwili iliyopita, alisema hakucheza mechi
za kirafiki na timu kubwa ili kuipima timu yake kutokana na jinsi
alivyoikuta ikiwa kwenye kiwango kidogo, hivyo alichokuwa akidili nacho
ni kuijenga icheze kitimu.
“Kwa ugeni wetu huu katika ligi, lengo
letu ni kubaki kwenye ligi na siyo kuwa mabingwa, nimefanya kazi kubwa
ya kuijenga lakini sijajua imejengeka kwa kiasi gani. Nitaijaribu kwenye
mechi nne za mwanzo wa ligi, kama bado nitaendelea kuzidi kuiimarisha,”
alisema Lonnstrom.

Note: Only a member of this blog may post a comment.