Saturday, September 19, 2015

Anonymous

Penzi la SHUMILETA Lamtesa TX Moshi Jr

shumileta 
Brighton Masalu
MAHABA niteketeze! Moshi William ‘Tx Moshi Jr’, mwimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma anaendelea kuwewesekea penzi la aliyekuwa mpenzi wake wa zamani ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’.
txjuniorAkizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, Moshi alisema ingawa kimepita kipindi kirefu tangu atengane na Shumileta, bado analikumbuka penzi la msanii huyo na kwamba alikuwa mwanamke mwema na mwenye kila sifa ya kuwa mke wa mtu na hujutia ni kwa nini alichezea bahati ya kumuoa.
“Dah, unajua nakumbuka mbali sana, hakika Shumileta alikuwa zaidi ya mwanamke, nalikumbuka penzi lake na mara nyingi huwa najutia ni kwa nini nilichezea bahati ya kumuoa mwanamke huyo, bado naumia sana,” alisema Tx Moshi Jr.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.