Breaking news! Saa chache kabla ya ile sherehe ya kukata na shoka ya
40 ya mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’ inayotarajiwa kufanyika mapema kesho,
ndani ya familia hiyo kunadaiwa kuibuka bonge la mpasuko.
Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na mtoto wake.
Habari kutoka kwa chanzo makini ndani ya familia hiyo yenye maskani
yake nje kidogo ya Jiji la Dar, maeneo ya Madale-Tegeta zilieleza kuwa,
kuna madai mazito ya usengenyaji ambayo yametawala yanayodaiwa kutia doa
katika shughuli hiyo ya kesho.
NI MAMA DIAMOND NA ZARI
Habari hizo za kidaku zinadai kwamba, mama mzazi wa Diamond, Sanura
Kassim ‘Sandra’ yuko kwenye sintofahamu na mwandani wa mwanaye, Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mambo ya
umbeya.
KAMERA ZABUMBURUA
Chanzo hicho kimelieleza gazeti hili kuwa, hivi karibuni, Zari,
kupitia kamera za ndani ya nyumba hiyo, Close Circuit Television (CCTV),
alibaini picha zikimuonesha Mama Diamond na mwanaye wa kike ambaye ni
dada wa Diamond aitwaye Esma Platnumz wakiwa kwenye mazungumzo na
muonekano wa kumseng’enya, jambo ambalo lilimkera kupitiliza.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mtoto wake Princess Tiffah.
ZARI ATAKA KUONDOKA NA TIFFAH
Mpashaji huyo aliendelea ‘kuponyokwa’ na maneno kuwa, baada ya
kubaini jambo hilo, Zari amekuwa katika harakati za kutaka kuondoka
nchini kwenda kwao kwa kile alichokiita ‘kujiepusha na ya walimwengu’
kabla hata mwanaye, Tiffah hajafanyiwa pati yake ya kutimiza siku 40
tangu kuzaliwa kwake.
“Hapa nyumbani hali si shwari kabisa, Zari hajapendezwa na kitendo
hicho, siku zote amekuwa akiishi nao kwa upendo akiamini ni watu wema
kwake, sasa anashanga tena kuwepo kwa hali ya majungu na manenomaneno.
“Nasikia amefikia hata hatua ya kulazimisha kuondoka Bongo na mwanaye,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.
“Nasikia amefikia hata hatua ya kulazimisha kuondoka Bongo na mwanaye,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.
Zarina Hassan ‘Zari the bosslady’.
MPASUKO?
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, kitendo hicho kimesababisha
mpasuko mkubwa kwenye familia ya Diamond kwani kuna baadhi ya
wanafamilia wapo upande wa Zari na wengine wapo upande wa Mama Diamond
na Esma.
HUYU HAPA MAMA DIAMOND
Baada ya kujazwa ubuyu huo wa motomoto, muda mfupi kabla ya kwenda
mitamboni, gazeti hili lilimtafuta Mama Diamond na kumuuliza juu ya ishu
hiyo ambapo alikanusha vikali kwa madai kwamba hayo ni maneno ya umbeya
kisha akakata simu.
MAMA DIAMOND ADONDOSHA KIMOMBO
Hata hivyo, alipoendelea kupigiwa ili afafanue maswali ya mwandishi, Mama Diamond alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa kimombo.
Mama Diamond: Iam driving (naendesha gari).
Mama Diamond: Iam driving (naendesha gari).
MAANDALIZI YA SHUGHULI USIPIME
Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, maandalizi ya shughuli ya Tiffah
yalikuwa yamekamilika kwa kila kitu huku ndugu wa Zari wakiwa
wameshafika nyumbani hapo wakiongozwa na Mama Zari, Halima Hassan.
Hatimaye, Diamond na Zari walifikia makubaliano ya kufanyia shughuli hiyo nyumbani hapo baada ya kuwepo kwa msuguano mkali kufuatia makampuni ya bidhaa za watoto kutaka ifanyikie kwenye ukumbi.
Hatimaye, Diamond na Zari walifikia makubaliano ya kufanyia shughuli hiyo nyumbani hapo baada ya kuwepo kwa msuguano mkali kufuatia makampuni ya bidhaa za watoto kutaka ifanyikie kwenye ukumbi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.