Nyuma ya safari za mara kwa mara za Mbongo fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ za nchini Nigeria, kumeibuka madai mazito kuwa,
anapokwenda huko hufundishwa mbinu za uchawi ili kukubalika duniani kama
mastaa wa huko, Risasi Jumatano limenyetishwa.
Ilidaiwa kwamba, mila na desturi za nchi hiyo zimeelekezwa zaidi
katika mambo hayo hivyo hata wasanii wake maarufu wanadaiwa kuegemea
humo.Kuhusu hilo, bila kutaja majina, ilidaiwa kwamba, kuna baadhi ya
wasanii waliotenga vyumba maalum ambako wameweka vitu vyao
vinavyohusiana na mambo hayo na huwa wanaviamini kuwa vinawasaidia
kuwika kwenye ulimwengu wa sanaa.
DIAMOND ANAHUSISHWAJE?
Kutokana na ukaribu wake na baadhi ya mastaa wa Nigeria, Diamond anatajwa kuelekezwa kwa ‘mafundi’ wa huko.
“Unajua wanasema kila mgeni lazima awe na mwenyeji. Kwa hiyo jamaa zake wa kule ndiyo humwelekeza walipo mafundi,” kilisema chanzo kimoja.
“Unajua wanasema kila mgeni lazima awe na mwenyeji. Kwa hiyo jamaa zake wa kule ndiyo humwelekeza walipo mafundi,” kilisema chanzo kimoja.
TUZO ZATAJWA
Ilisemekana kwamba, kutokana na suala hilo ndiyo maana Diamond
anazidi kupasua anga kwenye ulimwengu wa muziki akiipaisha vyema Bongo
Fleva na kuzoa tuzo kibao za kitaifa na kimataifa na kupata shavu la
kufanya kazi na wasanii wakubwa wa Marekani kama Shaffer Chimere Smith
‘Ne-Yo’.
HE! KUMBE ZARI ANA UKARIBU NA WANIGERIA!
Ikadaiwa kwamba, hata utajiri alionao na mafanikio ya mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ chimbuko lake ni hukohuko kwani naye ana ukaribu mkubwa na mastaa wa Nigeria na amekuwa akifanya nao biashara mbalimbali lakini bila kuwekwa wazi masuala ya ndumba.
Ikadaiwa kwamba, hata utajiri alionao na mafanikio ya mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ chimbuko lake ni hukohuko kwani naye ana ukaribu mkubwa na mastaa wa Nigeria na amekuwa akifanya nao biashara mbalimbali lakini bila kuwekwa wazi masuala ya ndumba.
Mastaa wa Nigeria ‘Naija’ wanaotajwa kuwa ndiyo huwa wenyeji wa
Diamond na wengine ameshafanya nao kazi ni pamoja na Peter na Paul Okoye
(P-Square), David Adedeji Adeleke ‘Davido’, Kingsley Chinweike Okonkwo
‘KCEE’, Yemi Alade, Tiwa Savege, Oladapo Daniel Oyebanjo ‘D’Banj’ na
wengineo ambapo mara tu anapotua Nigeria humpokea na kumpa kampani hadi
anaporudi Bongo.
DIAMOND ASAKWA, YUPO NIGERIA
Kufuatia madai hayo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Diamond kwa njia
ya simu ambapo lilielezwa kuwa yupo nchini Nigeria ambako ana
‘projekti’ mpya na baadhi ya mastaa hao wakiwemo D’Banj na Omotola
Jalade Ekeinde.
Risasi Mchanganyiko liliamua kumtumia meseji kupitia Mtandao wa WhatsApp na kumuuliza maswali mawili.
Risasi Mchanganyiko liliamua kumtumia meseji kupitia Mtandao wa WhatsApp na kumuuliza maswali mawili.
Kwanza lilimuuliza kuhusu madai hayo ya kufundishwa ndumba Nigeria,
pia lilimuuliza kuhusu madai ya mtangazaji Loveness Malinzi ‘Diva’
kusisitiza kuwa, kufuatia ugomvi wake na Diamond kwa kumtukana ndani ya
studio wiki iliyopita, hawezi kumsamehe, anamburuza kortini.
“Mimi nasoma kwako kwamba atanipeleka kortini. Mimi sijapata barua yoyote ile ya kuitwa huko kortini.”
AMEWAHI KUTAMKA
Hata hivyo, mara kadhaa, Diamond yeye amekuwa akikanusha vikali juu
ya ishu hiyo ya kutumia uchawi kwenye sanaa akisema kuwa hakuna kitu
kama hicho na huwa anamwamini Mungu na anaswali swala tano.
“Mimi namtegemea sana Mungu kwenye kazi zangu na bidii katika kazi
ndiyo maana hata nalala studio kwa sababu nataka nifike mbali kwenye hii
kazi hivyo nashangaa sana watu kuzusha kwamba natumia uchawi,” alisema
Diamond siku kadhaa zilizopita.

Note: Only a member of this blog may post a comment.