Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Bi. Celina Kombani umewasili muda huu katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Mwili
wa marehemu Kombani umewasili kwa ndege ya Shirika la Emirates,
ukitokea nchini India ambako alienda kutibiwa na mauti yakamkuta huko,
juzi Alhamisi.
Mwili umetolewa nyumbani kwa marehemu, Mikocheni, sasa umepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Lugalo ya jijini Dar.
Taarifa zaidi za msiba huu tutaendelea kukujuza.
PICHA NA DENIS MTIMA NA DEOGRATIAS MONGELA/GPL
Note: Only a member of this blog may post a comment.