Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM, Dk. John Magufuli.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM, Dk. John
Magufuli, amewashangaa watu wanaokejeli safari za nje za Rais Jakaya
Kikwete, akisema manufaa ya ziara hizo ni makubwa kuliko wanavyofikiri.
Amesema kupitia safari hizo, Rais Kikwete amefanikiwa kuwashawishi wafadhili kutoa misaada ya miradi mbalimbali nchini.
Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni katika kata ya Mvumi Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jana.
Dk. Magufuli alitoa mfano wa Sh. bilioni 992 zilizotolewa na
Serikali ya Marekani hivi karibuni kupitia mfuko wa MCC kwa ajili ya
miradi ya umeme kama sehemu ya matunda ya safari za Rais Kikwete nchi za
nje.
Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimelaani kitendo
kinachodaiwa kufanywa na wafuasi wa Ukawa kuvamia ofisi za chama hicho
mkoani Tanga na kufanya mashambulizi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM,
January Makamba, shambulio hilo lilifanywa juzi kabla na baada ya Ukawa
kumaliza mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tangamano kwa kurusha chupa
zenye haja ndogo.
Aidha, alidai kuwa tukio hilo lilifuatiwa na la mgombea wao wa
urais, Dk. John Magufuli, la kusimamishwa njiani na vijana wa Ukawa
pamoja na kupiga kelele kwenye mkutano wake wa hadhara mkoani Mbeya
kuwafanya wananchi wasimsikilize.
CHANZO: NIPASHE
Note: Only a member of this blog may post a comment.