Dustan Shekidele, Morogoro.
UTABIRI! Wakati taasisi mbalimbali zisizo za
kiserikali zikitoa matokeo ya utafiti katika kinyang’anyiro cha uchaguzi
mkuu mwezi ujao, kikongwe mmoja, Kete Abdallah mwenye umri wa miaka
100, amemtabiria ushindi mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
Bibi huyo alitoa utabiri huo wiki iliyopita wakati wa sherehe yake ya
kumbukumbu ya kuzaliwa iliyoandaliwa na wajukuu na vilembwe wake na
kufanyika nyumbani kwake, Ukonga jijini Dar es Salaam.Mmoja wa wajukuu
zake, Dustan Shekidele ambaye ni mwandishi wa gazeti hili, alisema
alimkuta bibi yake akiwa amelala kitandani akiwa amekumbatia redio na
alipomuuliza sababu ya kuwa hivyo, alidai anafuatilia habari za mgombea
huyo, kwani anaamini atashinda na endapo ataamka salama siku hiyo,
atampatia kura yake ya ndiyo.
“Unajua ukubwa dawa, najua kila mtu ana chama chake siwezi
kuwaingilia, lakini ninawashauri viongozi wangu wa CCM, uchaguzi wa
mwaka huu ni mgumu, upinzani umekuwa na nguvu,” alisema bibi huyo na
kuwashauri viongozi wa CCM kutembelea majumbani na mahospitalini
kuwabaini makada wa CCM ambao hawataweza kutoka kwenda kupiga kura.
Mmoja wa vilembwe wa bibi huyo, Tumaini Shekidele akisoma risala
kwenye sherehe hiyo, alisema bibi huyo alizaliwa Septemba 27, 1915
katika Tarafa ya Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga na kwamba hadi
sasa ana wajukuu na vilembwe 302.
Note: Only a member of this blog may post a comment.