Tuesday, September 22, 2015

Anonymous

Jibu la Mama DIAMOND Kuhusu Sura ya Mjukuu Wake, Udhamini wa TIFFAH je?, Maneno ya MBASHA Baada ya Kuachiwa Huru…#255

Weekend iliyopita mtoto wa Diamond na Zari aitwaye Tiffah alitimiza siku 40 na sura yake kuonyeshwa LIVE kwa mashabiki wao..255 ikaamua kupiga stori na mama Diamond kujua anazungumzia nini kuhusu mjukuu wake kudaiwa si damu yake..amesema yale yalikuwa ni maneno ya Magazeti..anasema Mungu kawafedhehesha wote waliokuwa wakisema hivyo kwa kuwa mjukuu wake ni kopy ya Diamond kuanzia pua, mdomo macho na pia anatabia zote alizokuwa nazo Diamond.Diamond amesema kama mzazi lazima ajue jinsi ya kuwa mbunifu kwa kutumia kampuni kubwa kama ambavyo amefanya kwa mwanaye, anasema mtoto akiwa balozi wa kampuni yoyote inasaidia sana katika kupunguza gharama na hata kumsaidia katika maisha yake ya baadaye.

Diamond akiwa amembeba Tiffah
Mahakama ya mwanzo ya Ilala leo imemwachia huru Mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha ambaye alikuwa na tuhumu za kesi ya kumbaka shemeji yake…amefunguka na kusema Mungu ni mwema ameshinda kesi, anamshukuru sana Mungu, anawashukuru Watanzania wote kwa kumuombea kwa kuwa alikua kwenye mapito magumu sana katika maisha yake.
Wasikilize hapa…

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.