Imelda Mtema
FUNGUKA! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’
amesema anakasirishwa na ‘wambeya’ ambao kila uchwao wamekuwa
wakimuuliza atarudi lini kwa mumewe, Abdallah Shakoor ambaye
walitengana miezi kadhaa iliyopita.
“Yaani unamkuta mtu anajadili juu ya mimi kurudi kwenye ndoa yangu na wakati nilivyoondoka hakuna yoyote aliyefahamu hivyo siku ambayo nitaona inafaa kurudi kwenye ndoa yangu, nitarudi na watu watashtukia nimerudi tu mwenyewe bila shuruti ya mtu,” alisema Davina huku akiahidi kuwataja majina wambeya hao kama wataendelea kumsema.
Note: Only a member of this blog may post a comment.