Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba akivuta ‘mambo’ (shisha).
Dustan Shekidele, Moro
KATIKA hali isiyo ya kawaida
wananchi mkoani hapa wamejikuta wakipigwa butwaa mara baada ya
kumshuhudia staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba akivuta ‘mambo’ (shisha)
kisha ‘kuzima gari’ ukumbini.
TUJIUNGE ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililopigwa chabo na
mwanahabari wetu lilijiri mishale ya saa 8:00 usiku wa Jumamosi
iliyopita katika ukumbi wa kisasa wa burudani wa Samaki Sport mjini hapa
ambao kulikuwa na nyomi la kufa mtu.
Awali, baadhi ya wananchi walimpiga
chabo Kiba kisha kumtonya paparazi wetu ambaye alifika fasta ndani ya
kiwanja hicho na kumshuhudia laivu msanii huyo akiwa na demu mwingine
mkali aliyejitambulisha kwa jina la Asia Mujuni na siyo Jokate Mwegelo
‘Kidoti’ ambaye amekuwa akifuatana naye kila sehemu katika siku za hivi
karibuni.
JOKATE UPO?
Baadhi ya watu wanajua uhusiano wa Kiba na Jokate walidai kuwa kama mwanadada huyo angekuwepo eneo la tukio pangechimbika.
WAVUTA KWA ‘KUSHEA’
WAVUTA KWA ‘KUSHEA’
Wawili hao walikuwa wakivuta shisha kwa ‘kushea’ huku Asia akishushia na kinywaji kikali.
Hata hivyo, Kiba awali hakumgundua
paparazi wetu hadi alipotonywa na msanii mwenzake, Stanley Yusuf ‘Stan
Bakora’ ambaye anamfahamu fika mwandishi wetu.
Kiba aliyeonyesha kama amezidiwa nguvu
kwa kilevi hicho, baada ya kutonywa alishtuka kisha akamchukua ‘patna’
wake huyo na kujikokota hadi kwenye gari ambapo walitokomea
kusikojulikana.
MASTAA WENGINE WALIOKUWEPO
MASTAA WENGINE WALIOKUWEPO
Kabla ya kutimua, kwenye meza aliyokaa
Kiba na mrembo pia kulikuwa na wasanii wengine kama Fareed Kubanda ‘Fid
Q’, Esterlina Sanga ‘Linah’ na Kibwana Saleh ‘KB’ ambaye maskani yake ni
mjini hapa.
Akizungumza na gazeti hili, KB ambaye
pia alikuwa akivuta shisha alimtetea Kiba: “Kiba ni ndugu yangu na haya
siyo madawa, ni shisha, Ulaya mastaa wanavuta. Baadhi ya watu humu
ukumbini wanadai ni madawa ya kulevya lakini siyo kweli huu ni moshi wa
kawaida.”
Naye mmoja wa mashabiki wa Kiba, Jumanne
Idd aliyezungumza na gazeti hili kuhusu ishu hiyo alifunguka: ”Kila
siku tunakuja kwenye kiwanja hiki cha Samaki, hatujaona watu wakivuta
shisha humu ukumbini. Leo ndiyo tumemshuhudia Kiba kufuatia moshi wa
kilevi hicho kuwa mkali, ilibidi mimi na demu wangu tuhame meza.”
Kijana mmoja wa mjini aliyefahamika kwa
jina la Juma lssa alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema: “Ni kweli
kifaa kile ni moshi wa kawaida lakini kuna baadhi ya watu wanachanganya
na moshi wa bangi.”
KIBA ATAFUTWA
Jitihada za kumtafuta Kiba ili kuzungumzia ishu hiyo ziligonga mwamba na hata alipotafutwa kwa njia ya simu haikuwa hewani.
Shisha ni kiburudisho ambacho kimekuwa
maarufu sana miongoni mwa mastaa na vijana wengine wa daraja la kati
ambao hukitumia, hasa sehemu za starehe nyakati za usiku na mikusanyiko
mingine ya burudani inayojumuisha watu wengi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.