Wednesday, September 9, 2015

Anonymous

ALAMA ZINAZOTUMIWA NA FREEMASONS


Mpenzi msomaji wiki iliyopita niliishia pale nilipokuwa nikizungumzia vikao vya Freemasons ambapo huwa mwenyekiti wao wanamwita Master na anakuwa na wasaidizi wawili. Kwenye ibada zao mwenyekiti huwa anakaa upande wa Mashariki, msaidizi mmoja anakaa mbele yake akimtazama na mwingine anasaidia shughuli nzima inayoendelea. Kunakuwa na mtu mwingine ambaye ndiye mwongozaji wa sala na wakati wakisali huwa Mungu wanamwita Fundi Mkuu aliyeumba sayari zote.
SASA ENDELEA...
Freemasons huwa wana alama au nembo (siyo ishara) ambazo huwatambulisha jamaa hao. Kuna alama ya compass inayotumika kuonesha mwelekeo kwa mishale yake, kuna rula na pembenne ambavyo ni vitu vinavyotumika kwenye ujenzi ila vinaweza kutumika kufundisha kuhusu maisha na ndivyo vinatumika hivyo wala siyo kuhusu kitu kingine.

Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilikuwa ni kundi la mafundi waashi (masoni) au wajenzi kwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalam waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa Kizungu (medieval times).

Walikuwa ni watunzaji wa fedha za Kanisa Katoliki. Kwani walikuwa wanajenga mahekalu (cathedrals) za Wakatoliki na mabenki, mahandaki ya kuhifadhia fedha pamoja na kuzikia (catacombs).

Walikuwa wanaweza kujenga hayo mahandaki kwa utaalam mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani, unaweza ukashindwa kutoka, unaweza kupotelea humohumo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalam wao.

Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi kama tulivyoona awali.

Wakati wakifanya ibada zao au kumkubali mtu kujiunga na Freemasonry, lazima mwanachama avae pajama au mavazi yanayotumika kulalia usiku na hawaruhusiwi kuwa na fedha mfukoni, kuvaa saa au cheni, ishara ya kuwa wao ni maskini kama walivyozaliwa.

Kunakuwa na mambo ya uchawi, kuabudu shetani na mambo kama hayo watu wanayosema kwamba Freemasons ndiyo hujihusisha na hivyo vitu ikiwemo kutoa uhai wa ndugu lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha kuwa ni uongo, hawana ujuzi wa kutosha.

Kuna maelezo kuwa aliyewahi kuwa Rais wa Kenya, Daniel Arap Moi aliwahi kuunda kamati maalum kuchunguza uchawi na waabudu shetani na ambapo Freemasons walihojiwa, ingawa hawakutoa ripoti kamili.

Baadaye kamati hiyo ilieleza kuwa ilijiridhisha na kukubali maelezo yao na ingekuwa bora kama watu wangewaelewa zaidi ili kusiwe na mambo ya siri.

Kuna faida yoyote ya mtu kuwa Freemason? Kwa maelezo yao wenyewe huwa wanasema hakuna faida za kupata fedha kama wengi wanavyoambiwa kwamba ukiwa Freemason unapewa fedha.

Faida ya kuwa Freemason ni pamoja na kuongeza idadi ya marafiki na kuongeza knowledge (ufahamu). Faida nyingine labda ni kama ukitoa tenda kama unaanzisha kiwanda na umetoa tenda ya kazi, ukiona mmoja wa Freemasons yuko kwenye listi ya walioomba tenda, utampa kipaumbele kwa sababu unamfahamu na ni kama ndugu.

Pia wenyewe wamekuwa wakikanusha vikali kwamba hakuna utoaji wa kafara kama inavyosemekana na pia hakuna uhusiano kati ya Freemasons na agano la kale.
Je, nini kitaendelea? Usikose wiki ijayo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.