Hivi elimu yetu inatuandaa kuwa tutakapomaliza tuwe chini ya mabosi tutakao wakuta kazini, elimu gani hiyo inashindwa kuikomboa jamii inayokuzunguka..elimu isiyoweza kuajiri hata watu 5...angalia hata kwenye fani zetu uigizaji,mziki,watangazaji hata waandishi wasomi wengi hawapo na watu wanafanya vizuri..ingawa sasa tunahitaji mbinu mpya toka kwao...mzungu alichukia akasema machinga wana mbinu mpya kuliko hawa...
Akosee mtu kizungu utawaona heee wasanii hawajasoma...jiulize elimu yako imelisaidia nini taifa...Sisi wengi wetu ni form4 lakini tumetoa ajira kubwa kwa watu..wasanii,machinga,maduka mengi tu ingawa tuna mapungufu mengi...wasomi njooni tusaidiane huku pia kuna pesa amkeni.
Jacob Stephen ‘JB’ @jb_jerusalemfilms on instagram

Note: Only a member of this blog may post a comment.