Friday, August 7, 2015

Anonymous

UMEJIANDIKISHA KUPIGA KURA? TAARIFA HII YA MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI NI MUHIMU SANA KWAKO, ISIKUPITE

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Ramadhani Kailima Kombwey (pichani juu) amesema hakuna sharia inayomlazimisha mtumishi wa umma kusalimisha kadi yake ya kupigia kura kwa mwajiri wake.

Mkurugenzi huyo amesema kwa mijibu wa sheria ya taifa ya uchaguzi, hairuhusiwi na haitakiwi kwa mtu aisiyehusika na kadi ya mpiga kura kuimiliki kadi hiyo.

Ramadhani Kailima amesema kufanya hivyo ni sawa na kujiandikisha mara mbili ambayo ni kosa la jinai.

Aidha, Kailima ametahadharisha kuwa ni makosa kwa mtu mwingine asiyekuwa mtumishi wa Tume ya uchaguzi kutaka kupata taaraifa ya kadi ya mpiga kura mwingine.

“Wapiga kura wasikubali popote pale walipo, kwa chombo chochote kile kisichokuwa tume kuomba kupata namba ya mpiga kura au kupata kadi ya mpiga kura.
“Iwe taasisi, kiwe chama cha siasa, iwe asasi, chochote hata baba yake asikubali kumpa kadi yake ya mpigia kura,” alifafanua Kailima.
Tunaomba maoni yako kuhusiana na habari hii.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.