Karibu
msomaji wangu katika ukurasa huu ambao tumekuwa tukifundishana mengi
yahusuyo afya zetu na tukipeana elimu ya kuboresha afya zetu.
Wiki iliyopita tuliangalia tatizo la mwanamke kukosa hedhi na tukazipitia baadhi ya sababu au vyanzo vya mwanamke kukosa hedhi.
Leo ningependa kuhitimisha katika kipengele cha vyanzo vya wanawake wengi kukosa hedhi.
Ningependa kuwatoa hofu wasomaji wa makala haya kuwa kukosa hedhi siyo ugonjwa ni matokeo au dalili za tatizo fulani katika mfumo wa uzazi ni vema mwanamke anayeona ana tatizo hilo awahi katika vituo vya afya ili afanyiwe uchunguzi na kupatiwa matibabu ya tatizo lake. Pamoja na kuangalia vyanzo vingi vya tatizo hili la mwanamke kukosa hedhi kuna sababu nyingine ambayo leo ningependa tuiangalie vizuri huenda ikakusaidia chanzo cha tatizo lako.
Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi:
Kuna wakati mwanamke akijitazama anajiona yupo sawa kabisa na haoni kama kuna kasoro yoyote katika maumbile yake labda kasoro ziwe ni za sehemu ya nje ya via vya uzazi. Ikumbukwe kuwa uzazi ni mfumo unaohusisha viungo ili ufanye kazi sawasawa kabisa
Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na:
Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke.
Kuta za ‘uterus’ zinazotazamana kujishikiza pamoja.
Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen).
Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka.
Pia kuna baadhi ya mambo ambayo pia yanaweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na:
Unene uliopitiliza au kupungua uzito/ kukonda isivyo kawaida.
Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu, utapia mlo na msongo wa mawazo.
Matumizi ya baadhi ya madawa hususan baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili.
Kuwa na hofu iliyopitiliza.
Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi.
Kwa jumla pamoja na sababu nyingi za mwanamke kukosa hedhi hizi ni baadhi yake. Na kuna dalili mbalimbali zinazoweza kutumika kutambua kuwa mwanamke husika ana tatizo husika la kukosa hedhi. Lakini kumbuka kuwa suala la hedhi ni pana unapoona hedhi yako haipo sawa ni vema ukawahi kuwaona wataalamu wa afya ya uzazi ili wakusaidie kufanya uchunguzi na kukutafutia matibabu ya tatizo lako kulingana na chanzo cha tatizo. Lakini pia unaweza ukatembelea Sigwa
Herbal Clinic kwa uchunguzi na matibabu ya uhakika.
Saturday, August 1, 2015
Sababu za Mwanamke Kukosa Hedhi-3
Tutaendelea wiki ijayo.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
MAKALA
on Saturday, August 1, 2015

Note: Only a member of this blog may post a comment.