Habari kuhusu ujio wa collabo kati ya superstar wa Nigeria, Davido
na superstar wa Tanzania Alikiba tuliisikia kutoka kwa Davido mwenyewe
wakati wa tuzo za 2015 MTV MAMA zilizotolewa huko Durban, Afrika Kusini.
Hatimaye Alikiba naye amezungumzia collabo hiyo kwa mara ya kwanza,
kwa kuthibitisha kuwa alichokisema Davido ni kweli hivyo watu wajiandae
kupokea kazi hiyo hivi karibuni.
“Davido ameongea na Millardayo kwamba anataka kuja kufanya
featuring na Alikiba, which is tayari tulikuwa tumeshaongea muda mrefu,
kwahiyo watu wasubirie tu ngoma inakuja kutoka lini.
Alisema King Kiba kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
Alikiba pia ameelezea kile ambacho wanatarajia kukiimba katika wimbo huo ambao bado haujarekodiwa.
“Track iko vizuri, lakini idea bado haijakamilika, lakini
kiukweli mi hua nafanya ngoma nikiwa studio, tutazungumzia kuhusu
goodtime, party, mapenzi flani you know, yaani nyimbo flani ya
kuhamaishisha watu katika raha.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.