MWANAMITINDO maarufu duniani, Naomi Campbell (45)
ametupwa jela miezi sita baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga paparazi,
Gaetano Di Giovanni, Agosti, 2009.
Naomi akiwa katika pozi.
Campbell alidaiwa kumpiga Gaetano Di Giovanni jichoni na mkoba wake
baada ya kupigwa picha akiwa na aliyekuwa mchumba wake wakati huo
August, 2009.
Mdada huyo ambaye ni mkongwe kwenye masuala ya mitindo, amehukumiwa
na Sicilian Court kifungo cha miezi sita jela, Ijumaa ya Julai 31, mwaka
huu lakini kifungo chake kinafahamika kama ‘Suspended Prison Term’
ambacho hataingia nyuma ya nondo kwa sasa.
‘Suspended Prison Term’ ni kifungo ambacho mshtakiwa haendi jela moja
kwa moja baada ya hukumu kutolewa, lakini akivunja sheria katika
kipindi hicho (miezi sita) ataenda moja kwa moja jela, na akimaliza muda
huo bila kufanya kosa wala kuvunja sheria basi anafutiwa mashitaka.
Hata hivyo, mwanasheria wa Naomi, Guido Carlo Alleva amefungukia kesi hiyo kuwa watakata rufaa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.