Nimepata nafasi ya kuona namna ambavyo wanachama wa DP (Democratic Party) wakimsindikiza mgombea wao wa Urais kwa mwaka 2015 Mchungaji Christopher Mtikila pamoja na mgombea mwenza Juma Mathew Juma kuchukua fomu ya uteuzi kugombea Urais katika ofisi za Tume ya Taifa ya uchaguzi.
Tayari kwenye post iliyopita tulikua na picha za Mgombea Urais Lyimo wa chama cha TLP aliechukua fomu mapema leo ambapo kila mmoja baada ya kuchukua amekua na kauli kwa vyombo vya habari, moja ya kauli za Mchungaji Mtikila ni hii hapa chini.
‘Mimi ndio mwanzilishi wa UKAWA toka mwaka 1986′
Mchungaji Mtikila akiweka Sahihi tayari kwa kuchukua fomu ya uteuzi wa Uras mwaka 2015
Mgombea mwenza Bw. Juma Mathew Juma naye aliweka Sahihi yake
Kabla ya makabidhiano kukawa na maelekezo ya uchukuaji wa fomu , George Kashura wa NEC hapa anatoa maelekezo hayo kwa wagombea
Mchungaji Mtikila akitoka nje ya ofisi ya Tume baada ya kukabidhiwa fomu
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Kailima Ramadhani Kombwey akijibu maswali ya Mchungaji Mtikila
Mchungaji Mtikila mbele ya waandishi wa habari
Safari ya kuondoka ikafika hapa Mchungaji Mtikila akiingia kwenye usafiri wake tayari kwa kuondoka

Note: Only a member of this blog may post a comment.