Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amemmwagia sifa lukuki Waziri wa Ujenzi, John Magufuli kwa kufanikisha ujenzi wa Barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa Kilomita 60, katika kiwango cha lami.
Membe aliitoa kauli hiyo hivi karibuni mkoani Lindi wakati Magufuli ambaye pia ni Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, aliyeambatana na rais Jakaya Kikwete kuizindua barabara hiyo baada ya kukamilika.
Akiwahutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika kushuhudia uzinduzi wa barabara hiyo, Membe alianza kwa kumpongeza rais Kikwete kuwa wamepata ‘jembe’ ambalo limefanikisha barabara hiyo, hivyo kuwa na uhakika wa kuvuna kura nyingi katika uchaguzi ujao.
“Nimpongeze ndugu Magufuli, Magufuli sifa zote nazimwaga kwako. Mwenyewe hataki kujimwagia, lakini nasema umepata mchapakazi hodari sana, aliyesababisha yote haya…nashukuru barabara zinazokwenda ukweni kule Nyasa kwenda Mtwara ndiye yeye amezisimamia.
“Na nashukuru pale palipobaki, hasa Mbinga kwenda Mbamba Bay atamaliza ili mwenzake nifurahi zaidi kwenda kwa wakwe zangu asubuhi na kurejea jioni, mheshimiwa rais nakushukuru, mheshimiwa Magufuli nakushukuru na mimi nawahakikishia kwa niaba wa wananchi wa Lindi, mtapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao,” alisema Membe.
Rais Kikwete ambaye pia barabara hiyo imewanufaisha wananchi wa maeneo hayo na kwa upande mwingine kukiwa ni nyumbani kwa wakwe zake, aliitumia nafasi hiyo pia kuwaaga wananchi baada ya kuwatumikia kwa takribani miaka kumi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.