Katika Jimbo la Nanyumbu, mkoani Mtwara, Willium Dua alitangazwa mshindi
kwa kupata kura 6,165 huku mpinzani wake wa karibu Yahya, Mhata akipata
kura 6,157.
Mbunge anayemaliza muda wake, Dastan Mkapa, alishika nafasi ya tatu
9,3945. Wengine ni Endrick Napacho kura 2,096, Majaribu Lupeto kura 931,
Uledi Mwanache 497 na Hassan Wema kura 296.
JIMBO LA KIBAMBA
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara,
ameibuka kidedea baada ya kupata kura 5,576 akifuatiwa na Issa Mtevu
kura 3,296.
Nafasi ya tatu ni John Hugo aliyepata kura 319 na Pendo Kujerwa alipata kura 309.
JIMBO LA KAWE
Kippi Warioba ameibuka mshindi baada ya kupata kura 5,212 akifuatiwa na
Coleman Massawe kura 4,280, Juma Pijei 2,497 na John Cornel kura 584.
Katika jimbo hilo, wanahabari Abdallah Majura na Jerry Muro wameangushwa.
JIMBO LA UBUNGO
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi, amepata aliongoza kwa
kura 6,068, Kalist Lyimo 2,808, Hawa Ng’humbi 1,772 na Jordan Balindo
kura 212.
JIMBO LA KINONDONI
Idd Azan amefanikiwa kutetea nafasi yake baada kupata kura 6,479,
Michael Wambura 1,212, Wangota Salum 1,149 na Joseph Mhonda kura 751.
JIMBO LA ILALA
Mbunge anayemaliza muda wake Mussa Zungu ametetea nafasi yake kwa kupata
kura 10,457 akifuatiwa na Mkuu wa zamani wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho
Gambo kura 2,038 na Waziri Kindamba kura 575.
JIMBO LA UKONGA
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa amepata ushindi wa kura 10,000 dhidi ya Raesh Patel kura 7,356 na Rober Masegesi kura 548.
JIMBO LA SEGEREA
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk.Milton Mahanga ameangushwa na Bonna Kaluwa kura 6965.
Dk. Mahanga alipata kura 2,381 na Scolastica Kevila kura 6,155.
SONGEA MJINI
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, ameibuka kidedea katika
jimbo la Songea Mjini kwa kupata kura 6,287 na kumshindwa mpinzani wake
wa karibu Waziri Nchi wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk.
Terezya Huviza, kura 5,600.
Mussa Gama alishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 1,278a
akifuatiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Namtumbo, Azizi Fakiri kura
1,101.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST), Erick
Mapunda alipata kura 908, Meneja Masoko wa Clouds FM Radio, Raymond
Mhenga 576, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Francis Miti kura 475 na Wakili wa
Kujitegemea Manispaa ya Songea, Sebastian Waliyuba kura 265.
JIMBO LA MAKETE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binillith
Mahenge, ametetea nafasi yake katika jimbo la Makete baada ya kuibuka
mshindi mwembamba.
Dk. Mahenge alipata kura 8,534 dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk.
Norman Sigala alipata kura 8,211, Bonic Muhami kura 500, Fabianus
Mkingwa, 466 na Lufunyo Rafael aliyepata 226.
JIMBO LA MUFINDI KUSINI
Katika jimbo la Mufindi Kusini lililokuwa na wagomba 14, Mendra Kigola
aliibuka kidedea baada ya kupata kura 7,511 akifuatiwa na na Dickson
Lutevele kura 3,210, Albert Chalamila kura 1,898, Marcelina Mkini 1,684,
Mary Miho 413, Antony Mpiluka 331 na Wendei Ng’ahali kura 298.
JIMBO LA MUFINDI MJINI
Cosato Chumi alipata ushindi kwa kupata kura 3,686, Zuberi Ngullo kura
700, James Mgimwa kura 408 na Benjamini Billali kura 312.
JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI
Jimbo la Mufindi Kaskazini,Mahmoud Mgimwa alipata ushindi wa kura
12,235, nafasi ya pili ikishikiliwa na Exaud Kighahe kura 2,343, Raphael
Kalinga kura 1520 na Godfrey Ngupula kura 980.
JIMBO LA ARUSHA MJINI
Mshindi ni Philemon Monaban (5,320) akifuatiwa na Justin Nyari (1894), Moses Mwizarubi (1005), Reuben
Mwiteni (171), Thomas Munisi (832),Victor Njau (752), Emmanuel Ole Njoro
(90),Mohammed Omary (171), Swalehe Kiluvia (446), Hamisi Migire (305),
Weraufoo Munisi (832) na Mustafa Panju (498).
JIMBO LA NGORONGORO
Mshindi ni William Ole Nasha (30,389), Elias Ngorisa (15,599), Dk.
Eliamini Taika (10,588), Saning’o Ole Telele (6,432), Patrick Kasango
(3,222) naJoseph Saitoti (2,384)
ARUMERU MANGHARIBI
Mshindi ni ni Loi Sabaya (10,321), , Furaha Lekoko , 8,450), Elisa
Mollel (3,253), Daud Molle (2,183), na Henry Mejooli (2,025) na 0
Osiligi Losai (1,206).
LONGIDO
Mshindi ni Joseph Kuruju (5,452), Lomayani Kodie (4,579) na Philip Kitaso (4,096).
Chanzo: NIPASHE


Note: Only a member of this blog may post a comment.