Tuesday, August 4, 2015

Anonymous

MASKINI MAMA NGWEA! Anamkumbuka Sana Mwanaye, Katika Nyimbo Zake Zote Kwake Hii ni Namba 1

Ingawa hatuko nae duniani lakini upendo wake pamoja na nyimbo zake bado upo kwenye hizia za wengi na ndio maana jina lake ni gumu kusahaulika miongoni mwetu, alikua rapper kwenye game ya bongofleva ambaye hakuwahi kuchokwa, namzungumzia marehemu Albert Mangweha.
Wakati muziki wa kizazi kipya unaanza ilikua ni nadra sana kukuta wazazi wakiwasupport watoto wao waliokuwa wakifanya muziki huo kwa kipindi hicho kwa sababu asilimia kubwa ya wazazi walikua wakiamini muziki huu ni wa kihuni.

Mama Mangwea
Kwenye hii post leo tuko na Mama mzazi wa Ngwea na anataja nyimbo zinazomvutia na anazozikumbuka kutoka kwa Ngwea, anasema >>’Naipenda She Got a Gwan kwa sababu inaonyesha upendo halisi jinsi mtu akiwa na mwenzi wake waone kuna hali ya kusameheana au kuchukuliana katika upendo na ndiyo maisha yanayoweza kuwa katika watu wawili wanapokua pamoja
Nilianza kuusikia kwenye radio baadae akaja hapa tukaongea nae tukamwambia wimbo wako kweli Noma umetoka vizuri akacheka kwa sababu yeye alikua mtu wa kucheka,ukimwambia kitu cha kufurahisha anacheka anasema poa tu mama

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.