MAPENZI! Staa wa sinema
za Kibongo, Jacqueline Walper ‘Wolper’, amezidi kujipambanua mapenzi
yake kwa mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Edward Lowassa kwa kusema; “nampenda Lowassa hadi naumwa.”
Akizungumzia mapenzi
yake hayo hivi karibuni, Wolper alibainisha kuwa Lowassa kwake ni zaidi
ya rais hivyo ndiyo maana alikuwa akimnadi hadharani kupitia mitandao
ya kijamii alipokuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hata alipohamia Ukawa.
“Nisiwe mnafiki, mimi nampenda Lowassa
yeye kama yeye na si chama. Nimemuweka kwenye profile yangu katika simu,
nikizima nikiwasha simu, namuona yeye. Huu ni uhuru wa kujieleza kila
mtu anaweza kujieleza anavyotaka, namsapoti Lowassa kila atakapokuwepo,”
alisema Wolper.
Note: Only a member of this blog may post a comment.