Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiwa na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
Musa mateja
Imevuja! Gumzo la ndoa ya staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate
Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ inadaiwa
kupigwa zengwe kama ilivyowahi kutokea kwa Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kufuatia madai ya mwanadada huyo kumtambulisha jamaa huyo kwao
kisha kukataliwa.
MINONG’ONO
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa wawili
hao, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wawili hao walihudhuria
kwenye harusi ya dada wa Jokate hivyo kuibua minong’ono kwamba huenda
harusi inayofuata itakuwa yao.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, habari mbaya ni kuwa baada ya
Jokate kumtambulisha Kiba kwa ndugu, jamaa na marafiki baadaye kumpeleka
kwao, wazazi wa mwanadada huyo walikuja juu wakidai jambo hilo
haliwezekani huku sababu nne zikianikwa.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
KIGEZO CHA DINI
Madai yalishushwa kuwa, sababu ya kwanza ni kwamba, familia ya Jokate
hasa wazazi wake ni watu walioshika sana Dini ya Kikristo (Kanisa
Katoliki) huku Kiba akiwa ni Muislam kama ilivyokuwa kwa Diamond
aliyeshindwa kumuoa Jokate kwa kigezo hichohicho.
NDOA ZA MASTAA NI TATIZO?
Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’.
Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’.
KIGEZO CHA KABILA
Kigezo kingine kilichotajwa ni kabila ambapo wazazi hao wanataka
Jokate aolewe na mtu wa kabila lake la Wangoni tofauti na Kiba ambaye ni
Muha.
Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
KIGEZO CHA BONGO FLEVA
Chanzo kilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, wazazi hao wanaamini kwamba baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva ni wahuni hivyo kuwawia vigumu kukubali binti yao kuolewa na Mbongo-Fleva.Pia habari za ndani zilidai kwamba, Jokate na Kiba walikuwa kwenye harakati za kuoana kabla ya mwaka huu kumalizika ila zengwe limekuwa kubwa upande wa familia hasa kwenye suala la dini ambapo kila mmoja amekuwa akitaka mwanaye abadili dini.

KAMA DIAMOND
“Unajua kilichompata Kiba ni kama kile kilichomfika Diamond kipindi kile alipotaka kumuoa Jokate.
“Ilikuwa ni ishu hiyohiyo ya dini maana wazazi wa Jokate walikuwa wakimwambia kila siku kama kweli anampenda mtoto wao basi abadili dini lakini Diamond hakuweza kufanya hivyo na kujikuta wakishindwa kufikia lengo la kufunga ndoa,” kilitambaa chanzo hicho.

KIBA KAMA KAWA
Kama kawaida yake, Kiba alipoulizwa juu ya ishu hiyo alikanusha
vikali akidai kwamba hajawahi kuwa na mipango hiyo na mrembo
huyo.“Ulishawahi kunisikia nikizungumzia ishu hiyo? Siyo kweli
bwana…hakuna kitu kama hicho,” alisema Kiba akionekana ‘kumaindi’ kwa
kuulizwa juu ya jambo hilo.Kwa upande wake Jokate hakupatikana hewani na
hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu hivyo jitihada za kumpata
zinaendelea.
TUJIKUMBUSHE
Kwa muda mrefu, Jokate na Kiba wamekuwa wakiripotiwa kuwa ni wapenzi
lakini Kiba amekuwa mstari wa mbele kukanusha huku Jokate akikiri kuwa
jamaa huyo ni mtu wake.
Note: Only a member of this blog may post a comment.