Imelda Mtema
KAZI ipo! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Walper ‘Wolper’ kuamua kushonesha vazi maarufu (gwanda) la Chama cha Demokrasia na Maendeleo, chama ambacho mfuasi wake, Edward Lowassa amejiunga nacho Jumanne iliyopita.

Mara baada ya Lowassa ambaye aliyekuwa
mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM kuhamia Chadema kinachounda umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), Wolper alitangaza kusaka fundi wa gwanda
katika mitandao ya kijamii, akafanikiwa.
“Nina furaha ya aina yake, baba
(Lowassa) katoka CCM nami naungana naye katika maisha mapya ya Chadema
hivyo nimeshapata fundi, ananishonea gwanda soon nalitinga,” alisema
Wolper.

Note: Only a member of this blog may post a comment.