Deogratius Mongela na Chande Abdallah
NOMA! Waigizaji wa
filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Ester Kiama ambao
wanaripotiwa kama wapenzi, hivi karibuni walilazimishwa kwenda kupima
afya, ikiwa ni sharti lililotolewa na mke wa muigizaji huyo ili aweze
kurejea nyumbani baada ya kuondoka kwa wazazi wake.
Inadaiwa kuwa Dude amekuwa akifanya juhudi kubwa kumrejesha mkewe nyumbani, kitu ambacho alifanikiwa, lakini akipewa sharti kuwa ni lazima kama kweli wamechepuka na hawakutumia kinga, wapime ngoma na majibu apewe kuthibitisha ubora wa afya yake.
Ili kuhakikisha anamrejesha mkewe kwenye himaya yake, Dude alimshawishi Ester kwenda kupima afya zao, zoezi lililofanyika kwenye zahanati moja iliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam siku ya Sikukuu ya Nanenane.
Dude alithibitisha kupata vipimo vya afya katika zahanati hiyo baada ya kuulizwa, lakini akakanusha kama zoezi hilo lilitokana na shinikizo kutoka kwa mke wake.
“Ester alikuwa ananipa tu kampani, lakini mimi ni kawaida yangu kucheki afya, nashukuru Mungu majibu ni mazuri ila uzito ndiyo mkubwa nina kg 110, nimeshauriwa nipunguze uzito,” alisema Dude
Mkewe hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia suala hilo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.