Klabu ya Arsenal ya Uingereza ambayo ipo katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anaekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema, dalili za Arsenal kuongeza nguvu ya kumtaka mshambuliaji huyo zinazidishwa na kauli ya mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo Thierry Henry.

Thierry Henry
Arsenal imefanya usajili mkubwa mmoja tu katika majira haya ya usajili kwa kumsajili aliyekuwa kipa wa Chelsea Peter Cech lakini Henry anaamini kama itamsajili Benzema inaweza kurudi katika mbio za kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza toka ishinde taji hilo msimu wa 2003/2004.

Thierry Henry
“Nafikiri wanaweza fanya vizuri mwaka huu kama hawatakuwa na majeruhi, Giroud pekee kama mshambuliaji huwezi shinda taji, unahitaji aina nyingine ya mshambuliaji nafikiri Giroud anafanya vizuri kiukweli ameshinda magoli 14 katika mechi 18 hicho ni kitu kizuri sana”>>>Henry
“Lakini wakati mwingine unahitaji aina tofauti ya mshambuliaji na nafikiri huenda watampata Benzema bado wapo katika nafasi ya kuwania taji la Ligi Kuu na Ligi ya mabingwa “>>>Henry

Karim Benzema
Licha ya kukiri Arsenal ipo vizuri na inahitaji kujiimarisha kwa kumsajili Benzema lakini amekubali wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kama watafanya hivyo ila la Ligi ya Mabingwa ni ngumu kushinda taji hilo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.