Mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry ambaye kwa sasa
ni mchambuzi wa soka katika kituo cha SKY Sport, amesema anaamini kwa
kipindi hiki kilichobaki kwenye dirisha la usajili, ni lazima Arsenal
isajili striker na midfielder.
Alisema hayo jana wakati wa mechi kati Arsenal na Liverpool
iliyochezwa katika uwanja wa Emirate na kumalizika kwa sare ya bila
kufungana.
“Nadhani itakua ni wiki kubwa sana, swali ni kwamba watanunua
mchezaji, walikua wanakosa wachezaji sana leo usiku, bado wanahitaji
holding midfielder na striker pia. Tulikua tunasema hivi tangu mwanzo wa
msimu,” alisema.
Katika mazungumzo hayo Henry alisema pia hakuna jinsi zaidi ya
kutumia pesa ili kupata mchezaji anayehitajika kama hayupo kwenye kikosi
hicho hivi sasa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.