Muimbaji wa kundi la rock la U2 na mwanzilishi wa One Campaign, Paul
David Hewson maarufu kama Bono amewakutanisha wasanii wa Afrika wakiwemo
Diamond, Banky W, D’Banj, Omotola, Waje na wengine kutengeneza remix ya
wimbo ‘Strong Girls’ ambao ni sehemu ya kampeni hiyo.
Mastaa hao wamekutana jijini Lagos, Nigeria.
Katika picha hiyo ya juu aliyoweka Banky W kwenye Instagram
ameandika: Lol.. how cool is it to be photo-bombed by BONO? emojiemoji
@diamondplatnumz @officialwaje bigups to @onecampaign for the “strong
girl” remix project we are all working on.”
Awali wimbo Strong Girls uliimbwa na wasanii wa kike tu wakiwemo Vanessa Mdee na Victoria Kimani.

Note: Only a member of this blog may post a comment.