MSOMAJI karibu tena kwenye ukurasa huu ambao tumekuwa tukipeana elimu juu ya matatizo mbalimbali ambayo yanaisumbua jamii yetu na ulimwengu kwa jumla.
Leo ningependa nitoe utangulizi wa mada ambayo itakuwa ikiwekwa katika ukurasa huu kwa majuma kadhaa yajayo. Mada yenyewe inahusu tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovari).Watu wengi wamekuwa wakisikia wengine yamewakuta na wengine hawajui lolote kuhusu tatizo hili. Niweke wazi kwamba katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kuna uvimbe mwingi ambao hutokea sehemu mbalimbali katika mfumo wao wa uzazi.
Kila sehemu ambayo uvimbe hutokea kuna sababu zake na dalili zake.Hivyo, ni vema unapofanyiwa uchunguzi hospitali ukaambiwa una uvimbe kwenye kizazi ni vema ukauliza uvimbe huo upo sehemu gani ili upate uelewa zaidi wa tatizo lako.
Kabla hatujaingia kwa undani kujadili tatizo hili ni vema tukapeana maelezo ya msingi ili kufahamu uvimbe huo hutokea sehemu gani, huitwaje na visababishi vyake.Uvimbe kwenye ovari hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke.
Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke hujulikana kama Ovarian Cyst. Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa umri wowote ule na mara nyingi huonekana kwa wanawake walio katika umri wa kushika ujauzito. Yaani kuanzia kupevuka
Ovari ni nini?
Kwa kawaida mwanamke anakuwa na ovari mbili katika mwili wake. Yaani moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto kwake. Ovari hizi hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus).
Ovari hizi za mwanamke huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum. Kisha mayai ya uzazi hukua ndani ya ovari ya mwanamke kwa kuchochewa na baadhi ya homoni. Mayai haya hukua na kukomaa baada ya kiwango cha kichocheo aina ya luteinizing hormone kuwa juu.
Mayai haya husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi kupitia kwenye mirija ya falopiani kwa ajili ya kwenda kujipachika.
Kama upachikwaji wa yai lililorutubishwa kwa mbegu za kiume (au kama yai la uzazi ambalo halijarutubishwa) hautafanyika, basi ndani ya wiki mbili, corpus luteum huanza kusinyaa na kupotea yenyewe na kusababisha kushuka kwa kiwango cha vichocheo aina ya progesterone na estrogen.
Kushuka kwa viwango vya vichocheo hivi husababisha mfuko wa uzazi kuanza kutoa mabaki ya kuta zake pamoja na yai la uzazi na hii ndiyo pale mwanamke anapopata damu za hedhi (menstruation).
Lengo la kuelezea suala hili la hedhi ni ili ujue umuhimu wa mayai ya mwanamke pamoja na kazi zake.
Nikukumbushe tu msomaji wangu kuwa Sigwa Herbal Clinic inafanya vizuri katika kutoa tiba ya magonjwa mbalimbali ambayo yameisumbua jamii kwa muda mrefu na imefungua matawi katika mikoa mbalimbali Tanga, Mwanza, Arusha, Kahama, Kigoma, Dodoma, Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam unaweza kututembelea kwa uchunguzi na matibabu.
Wiki ijayo tutaendelea na mada yetu na tutaanza kuchambua uvimbe mmoja baada ya mwingine.

Note: Only a member of this blog may post a comment.