Monday, August 3, 2015

Anonymous

DK. SLAA Hana Sababu ya Kususa Kisa LOWASA Amehamia CHADEMA!

Amani iwe nanyi! Ndugu zangu na wapenzi wa mabadiliko nchini kwa ujumla....!
Hivi kama Dr Slaa amehudhuria vikao vyote vya kamati kuu ya chama na waliafiki na kuridhia kumpokea ndugu EDWARD LOWASA,Wakaweka msharti ya kumpokea ikiwemo ni pamoja na kukuueleza umma ukweli juu ya kampuni hewa ya Richmondi na sababu ya kujiuzulu kwake uwaziri mkuu mwaka 2008.


Lowassa alikubaliana na masharti hayo na akatekeleza! Je, Dr Slaa kama mtu mwenye akili timamu na uelewa wake tunavyoujua alikua na sababu ipi ya msingi kususia wenzake! Kama ingekua ni kweli si angeiangikia kamati kuu barua juu ya kutokukubaliana na suala hilo?

Ninyi msiokua wanachadema nani kawapa mamlaka kujua na kumfuatilia Dr Slaa anafanya nini na yuko wapi? Anawahusu nini? Je, kama mwenyekiti anawaambieni anawasiliana naye mnataka nini zaidi? Mnajua wanawasiliana nini viongozi hao wakuu wa CHADEMA!
Mimi sio msemaji wa CHADEMA lakini sioni sababu ya msingi ya Dr Slaa kususa.

Toa maoni yako hapo chini tafadhali!
-JF

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.