Mrembo
wa Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ na Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, January Makamba wakipigana busu.
Musa Mateja
BUSU walilopigana
mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba lilizua gumzo la
aina yake huku wambea wakisema; “wamependezana.”
‘Katukio’
hako ka’aina yake kalitokea wiki iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar kulipokuwa na hafla ya umoja wa wasanii waliokuwa
wakimuaga Rais Jakaya Kikwete, anayemaliza madaraka yake, Oktoba 25,
mwaka huu.
Wakati
shamrashamra zikiendelea, muda wa kucheza muziki, Madam alikutana uso
kwa uso na Makamba ambaye anapenda kucheka na kila mtu, wakakumbatiana
na kubusiana ‘kiaina’ hali ambayo iliwafurahisha watu wengi.
“Wamependezana. Makamba mtu poa,
imenishtua kidogo walipochelewa kuachiana lakini najua ni salamu ya
kumisiana tu,” alisikika shuhuda mmoja.
Wawili hao kila mmoja ana mtu wake, kukumbatiana huko na kubusiana kulikuwa ni kwa kawaida tu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.