Msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ akibembelezwa.
WAANDISHI WETU
BONGE la soo! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza kufananishwa na marehemu Steven Kanumba.
BONGE la soo! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza kufananishwa na marehemu Steven Kanumba.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Posta, jijini Dar kulipokuwa na fainali za Shindano
la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki 10 ndiyo walikuwa
wakiwania kitita cha shilingi milioni 50.
Mara baada ya mshindi wa shindano hilo kutangazwa, ukumbi mzima
ulizizima kwa kelele za furaha na kwenda kumpongeza Dennis Laswai
aliyeibuka kidedea na wengi walikubaliana kuwa ni haki yake kutokana na
kufanya vizuri.
Ndipo ghafla, Ray ambaye alikuwa na upinzani wa kisanii na muigizaji
huyo, alipoanza kumwaga machozi hadharani na kujikuta amezungukwa na
watu wakimshangaa.
“Jamani mrithi wa Kanumba amepatikana rasmi baada ya miaka mitatu
kuishi bila yeye, sasa jembe limerejea tena, mama yetu hapaswi kuwa na
simanzi kila siku,” kijana mmoja alisikika akisema huku akienda kumshika
mkono mama Kanumba.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Ray baada ya mmoja wa vijana hao
kumfuata na kumuonesha fulana hiyo ambapo alizidisha kilio kiasi cha
wenzake kumfuata na kumtuliza ili awe katika hali ya kawaida.
“Ray hana lolote, pale amezidisha kiburudisho tu, hakuwa na mapenzi
na Kanumba kiasi hicho mpaka leo hii alie vile, ni usanii tu hakuna
lolote. Wapo watu wa kulizwa na kitu kama kile na si yeye, halafu Ray
huwa hana ushirikiano mzuri na wasanii wenzie hasa wa kiume,” alisema
mtu huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kwa upande wake Ray alisema kilichomtoa machozi ni ukweli kwamba
mshindi ana kipaji cha hali ya juu na yeye binafsi alipenda ushindi wake
kiasi kwamba mawazo yake yalimfikisha mbali.
Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Mayasa Mariwata na Musa Mateja.

Note: Only a member of this blog may post a comment.