Kocha wa timu ya vijana ya Azam,
Iddi Cheche akimuelekeza kwa vitendo mchezaji wake, Charles Stanslaus
‘Chale’ kabla ya kuingia uwanjani kuvaana na Ndanda FC.
Mchezaji wa Ndanda FC akisoma Gazeti la Michezo la Championi huku mchezo wa kirafiki kati ya timu yake na Azam ukiendelea.
Mchezaji wa Azam akiwa amepozi baada ya ‘warm up’ muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Ndanda.
Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha
vijana cha Azam wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya ‘warm
up’ kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Ndanda ya Mtwara uliopigwa leo.
Wachezaji wa Ndanda wakipasha
viungo kabla ya kucheza dhidi ya Azam katika mchezo wa kirafiki leo
asubuhi. Mchezo ulipigwa Uwanja wa Azam Complex. Ndanda walifugwa mabao
3-2.
Beki wa Ndanda, Paul Ngarema,
akipasha misuli kabla ya kuingia uwanjani kuiongoza timu yake kuvaana na
Azam katika mchezo wa kirafiki.
TIMU ya vijana ya Azam FC chini ya miaka 20 (U20) imewafanyia mbaya
Ndanda FC ya Mtwara inayoshiriki Ligi Kuu Bara baada ya kuifumua mabao
3-2 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Vijana wa Azam wanaonekana kuimarika kutokana na soka la kasi wanalocheza mwanzo mwisho.
Mchezo huo ulikuwa na kasi na ushindani, huku Azam wakijitahidi
kuzima mashambulizi ya Ndanda iliyosheheni wachezaji nyota akiwemo beki
na nahodha wa timu hiyo, Paul Ngarema.
(Picha/Stori: Nassor Gallu/GPL)
Note: Only a member of this blog may post a comment.