Licha ya kushindana yanapokuja maswala ya Tuzo, lakini kumekuwepo na
tatizo la kugeuza matokeo kuwa chuki kwa baadhi ya wasanii, kitu
ambacho msanii wa Nigeria Yemi Alade alifanya kinyume chake siku ya tuzo
za 2015 MTV MAMA.
Yemi Alade ndiye mshindi wa kipengele cha ‘Best Female’ alichokuwa anawania pia Vanessa Mdee.
Wakati wa kwenda kupokea tuzo hiyo Yemi aliwachukua wasanii aliokuwa
akichuana nao kwenye kipengele hicho, ambao ni Vanessa Mdee (Tanzania) ,
Seyi Shay (Nigeria), Bucie (South Africa) na Busiswa (South Africa) na
kwenda nao jukwaani kuashiria upendo na umoja licha ya yeye kuibuka
mshindi.
Kupitia ukurasa wake wa Insta Yemi aliandika kile kilichojiri baada ya jina lake kutajwa kuwa ndiye mshindi:
“Meneja wangu aliniambia simama kama mara tatu, ni kama
nililisahau jina langu mwenyewe…halafu mentors wangu Peter na Paul Okoye
wakanikumbusha natakiwa niende kupokea tuzo yangu…Lmaooo..
Isingewezekana kuwasahau dada zangu Seyi Shay, Vanessa Mdee, Bucie na
Busiswa, sisi ni nguvu moja, tunaenda pamoja.”
Kwenye post nyingine aliandika:
“I didn’t write a speech…”didn’t hezperetit” lol but everything
that came out from my mouth was to the glory of God alone…..
Dedicatedtotheteamthatneversleeps.#effyzziebaby ..#stronggirls and #
Mytangerines.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.