KUFUATIA kuwepo kwa makundi
yaliyotokana na watangaza nia 42 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa
wakiwania nafasi ya urais, mastaa waliokuwemo ndani ya makundi hayo
wameumbuka kufuatia ushindi wa John Pombe Magufuli, Risasi Mchanganyiko
lina ‘full’ stori.
WAMEUMBUKAJE?
Listi ndefu ya mastaa ikiongozwa na
Jacqueline Wolper, Wema Sepetu ‘Madam’, Wastara Juma, Kajala Masanja,
Elizabeth Michael ‘Lulu, Vincent Kigosi ‘Ray’, Jacob Stephen ‘JB’,
Bahati Bukuku, Tunda Man, Diamond na wengineo walikuwa wamegawanyika,
baadhi wakimuunga mkono Bernard Membe na wengine Edward Lowassa hivyo
alipopitishwa Magufuli ambaye hakuwa na wapambe, wakajikuta wameumbuka.
CHANZO CHASHUSHA UBUYU
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na
mastaa hao, kuumbuka kwao kulikuwa kwa aina mbili. Kuna baadhi
walikwenda Dodoma kulipokuwa kukifanyika vikao vya kuwachuja wagombea
wakiwa wamejiandaa kwa sherehe lakini kuna ambao walibaki Dar
kusikilizia.
“Walikwenda Dodoma wakiwa wameshahakikishiwa ushindi wa Membe na Lowassa, lakini bahati mbaya kwao hakukuwa na yeyote kati yao aliyefanikiwa kupenya, ingawa Membe aliingia Tano Bora,” kilisema chanzo chetu.
“Walikwenda Dodoma wakiwa wameshahakikishiwa ushindi wa Membe na Lowassa, lakini bahati mbaya kwao hakukuwa na yeyote kati yao aliyefanikiwa kupenya, ingawa Membe aliingia Tano Bora,” kilisema chanzo chetu.
KIZINGITI KILICHOWAKWAMISHA
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli na
Waziri Mkuu wa zamani, jina lake halikufanikiwa kuvuka kwenye Kamati Kuu
huku Membe ambaye ni Mbunge wa Mtama akiienguliwa katika mkutano wa
Halmashauri Kuu.
WALITINGA DOM KWA MBWEMBWE
WALITINGA DOM KWA MBWEMBWE
Chanzo kilizidi kumwaga ubuyu kuwa,
mastaa hao walitinga Dodoma kwa mbwembwe ikidaiwa kuwa
walishahakikishiwa ‘mtonyo’ baada ya mgombea wao kushinda.
“Ilikuwa wameshahakikishiwa ulaji. Wagombea wao waliposhindwa kuvuka, posho zao nazo zikayeyuka papo hapo.”
Kajala Masanja ‘Kay’.
KUMBE WALIANDALIWA SARE
“Yani ishu ilikuwa ni kubwa. Unaambiwa
waliandaliwa hadi sare kwa ajili ya kusherehekea ushindi lakini mambo
yote yaliharibika baada ya wagombea wao kushindwa,” kilieleza chanzo
hicho na kuongeza:
“Yaani waliumbuka kwelikweli maana kuna
ambao hawakwenda Dodoma lakini walikuwa wamewakilishwa na wenzao
walioenda na mikakati yao ilikuwa wangepita wagombea wao, wangeungana
kuwapigia kampeni nchi nzima.
WASIOKWENDA DODOMA
Risasi Mchanganyiko
limechimba wasanii ambao wanadaiwa kutokwenda Dodoma na kutajwa kuwa
wamewakilishwa na wenzao huku wakipiga kampeni kwenye mitandao ya
kijamii kuwa ni pamoja na Jacqueline, Wema, Lulu, Kulwa Kikumba ‘Dude’,
Bahati Bukuku na Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.
WALIOENDA DODOMA NI KINA NANI?
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa,
miongoni mwa wasanii waliokwenda Dodoma na kudaiwa kujipanga kwa sherehe
hizo za ushindi wa makundi ya wagombea ni pamoja na Steven Mengere
‘Steve Nyerere’, JB, Kajala, Ray na Wastara.
STEVE NYERERE AFUNGUKA
STEVE NYERERE AFUNGUKA
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya
Steve Nyerere ambaye alikanusha kuwepo kwa sherehe iliyopangwa lakini
aliungana na wenzake waliokwenda kumuunga mkono Membe lakini kwa kuwa
hakushinda, wamehamia kwa Magufuli.
“Sisi hatukuandaliwa sherehe, mimi JB,
Kajala, Ray na Wastara tulikwenda kumuunga mkono Membe na tulipewa
chetu, sasa kwa kuwa mgombea wetu ameshindwa tulihamia kwa Magufuli
ambaye ni timu moja na Membe,” alisema Steve.
Note: Only a member of this blog may post a comment.