Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando.
Shani Ramadhani
NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo,
Rose Muhando anadaiwa kumkimbia meneja wake, Alex Msama licha ya kuwepo
kwa makubaliano kati yao yaliyohusu kulipiwa deni la kiasi cha shilingi
milioni sita alizokuwa akidaiwa msanii huyo mwenye jina kubwa.
Alex Msama ambaye ni meneja wa Rose muhando.
“Meneja wake alikubali kumlipia pesa
zote (6,500,000) ambazo Rose alikuwa anadaiwa baada ya kushindwa
kuhudhuria tamasha moja huko mikoani, alitakiwa baada ya siku chache
aingie studio kufanya kazi, lakini ametoweka na haifahamiki yupo wapi,”
kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili lilimtafuta Rose bila mafanikio kwani simu yake haikuwa hewani.
Note: Only a member of this blog may post a comment.