Swali ambalo wengi wamejiuliza baada ya kuona vita ya maneno baina ya
Shilole na boyfriend wake Nuh Mziwanda katika mtandao wa Instagram , ni
je wanaachia lini wimbo mpya?
Ikimaanisha kuwa vita hiyo imetafsiriwa kama maandalizi ya kuachia
ngoma mpya huku wengine wakiamini kuwa huenda ukawa ndio mwisho wa penzi
lao.
Wakati wengine wakisheherekea sikukuu ya Eid weekend iliyoisha,
Muimbaji wa ‘Nakomaa na Jiji’ Shilole alitumia akaunti yake ya Instagram
kuandika vijembe kwa Nuh Mziwanda, alianza kwa kuandika:
“Mwanaume hata umfanyie nini haridhik lol! Pamoja na kukubali
shida zake zote lakin mh! Nimejitahid nimehangaika’ila sasa kama gari
limewaka’aka babu weeee kanikuta na maisha yangu wacha niendelee na
maisha yangu’Mimi na yeye baaaaaaasi #GaNdALaNdiZi”
Baada ya siku moja Shishi aliongeza kijembe kingine:
“Kidume unataka raha tu ‘pesa hauna ‘na bado siunaleta ujanja kwa
mtoto wa igunga ‘mjini hapa ‘halafu sina habari ‘wacha niwe busy na
kazi zangu tu’mapenzi yashanishinda mie.nawapenda sana mashabiki wangu!
Manopenda mitelemko kazi mnayo kupandisha vitonga hamtaki mtanyoookaa na
kama ulikuwa unatembelea Kik yangu basi katafute snare”.

Upande wa Nuh Mziwanda naye alijibu kupitia akaunti yake:
“Mwanaume wa kweli ukaa kimya’sibishani na upumbavu’mwanamke
asieridhika na kujua kua kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa’na kuvumilia
mambo yote alionifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu’familia
na’wasanii wenzangu na wadau’anaanza kunitukana mitandaoni for
whaaaat!!! Mxeeeeew’mimi bado kijana na nna time ya kupata maisha yangu
na mtu atakae thamini moyo wangu ‘nawaachia wanaume wenzangu na nyie
mjaribu zari ‘mimi nacheka tu #AsHaNgeDerE”
Kama ni ‘kiki’ ya wimbo wao mpya, unahisi hashtag walizotumia
#GaNdALaNdiZi na #AsHaNgeDerE zikawa zinahusika na jina la wimbo? Ngoja
tusubiri tuone!

Note: Only a member of this blog may post a comment.