Hivi kweli Malia Obama atakubali kupata mpenzi toka Kenya kisa baba yake ana asili ya huko?
Iliwahi kuchukua headlines stori ya
jamaa ambaye kazi yake ni Wakili, alitangaza kabisa mpaka posa ya
ng’ombe na mbuzi ambao amejipanga nao kutoa posa ili ampate Malia..
leo ni mwingine, kazi yake ni mfugaji na yeye kajiandaa kabisa na
ng’ombe kama 500 hivi alafu anasema hata zikitakiwa zaidi wako tayari
kuongeza.
>>>> ‘Tumekusanya
ng’ombe 500 wakitaka zaidi tuko tayari kutoa… sina mchezo kabisa niko
serious, hizi ng’ombe naweza kuzipakia kwenye meli na ziende‘>>>> Jeff Ole Kishau.
Basi akaulizwa kama ataweza kuongeana Malia kwa kiingereza, jibu lake hili hapa >>> ‘Najua kiingereza kidogo siwezi kushindwa.. naweza kuongea ‘YES how are you Malia’… ataelewa kabisa’ >>> Jeff Ole Kishau.
Unaambiwa hata ndugu na jamaa zake wanaamini jamaa atampata Malia Obama >>>> ‘Hata
yeye mwenyewe (Obama) ni damu ya Kenya, alienda Marekani akajenga
akapata familia mbegu ikaenea huko, tunaomba atupe huyo msichana ili
arudishe mbegu Kenya‘ >>>> Mmoja wa wazee ambao wanatoka Kijiji ambacho anatoka Jeff Ole Kishau.
Zimebaki siku chache Rais Obama atue Kenya, najua zitakuwepo stori nyingi kila wakati kwa sababu ya ugeni huo… nitahakikisha zote zinakufikia pia hapahapa mdau wangu.
Zimebaki siku chache Rais Obama atue Kenya, najua zitakuwepo stori nyingi kila wakati kwa sababu ya ugeni huo… nitahakikisha zote zinakufikia pia hapahapa mdau wangu.
Stori iko kwenye sauti hapa mtu wangu, nimeirekodi kwenye Habari ya K24 TV.
Hapa iko video pia ya story hiyohiyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.