Friday, July 24, 2015

Anonymous

RAIS BONGO MUVI: Sasa Naachia Ngazi!

mwakifwambaRais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Saimon Mwakifwamba katika ofisi za Global Publishers (Picha na Maktaba).
Imelda Mtema, Zanzibar
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Saimon Mwakifwamba amefungua kinywa chake na kusema kuwa mwaka huu lazima aachie ngazi ili awapishe wengine waendeleze gurudumu. 

Akizungumza na gazeti hili juzi mjini hapa, Mwakifwamba alisema kuwa muda aliokaa madarakani unatosha hivyo ni vyema akawapisha wengine wenye vigezo vya kuongoza.
“Watu wengi wanajua mimi sipendi kuachia ngazi, siyo kweli kabisa! Mwaka huu naachia ngazi ili mwingine aweze kuchukua kijiti. Najua wapo wenye nia thabiti ya kukuza tasnia yetu, nitawapisha,” alisema Mwakifwamba.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.