Friday, July 17, 2015

Anonymous

NAY WA MITEGO: Nina Maana Yangu Kutumia DAMU Kwenye Video Zangu!

Nay wa Mitego amesema kufanana kwa video ya wimbo wake ‘Sina Muda’ na ile ya ‘Mr Nay’ sio kitu cha bahati mbaya bali ni kunatokana na damu ambayo amekuwa akiitumia kama alama kwenye video zake.
IMG-20140725-WA0027 Nay wa Mitego akiwa katika utengenezaji wa video yake Mr Nay
Akizungumza na Clouds E ya Clouds TV, Nay amesema bado kuna video zinakuja zitakazokuwa na damu.
“Hii ni video ya pili naifanya hivi na kutakuwa na video nyingine ya tatu ambayo itakuwa na vitu kama hivyo,” alisema. “Hii ni kama sign yangu, kwahiyo nimepokea maoni mengi kuhusu kufanana kwa hii video lakini yote ni kwaajili ya damu na damu ni kama nilivyosema hii ni sign yangu,” aliongeza. 

Pia Nay alieleza sababu iliyofanya wimbo wake na Diamond, Mapenzi au Pesa kufeli.
“Ndio haujafanya vizuri lakini tukumbuke wimbo Mapenzi au Pesa ni wimbo ambao umekosa video. Kwenye muziki wetu wa siku hizi watu wanataka video haraka, ukichelewa kufanya video wimbo unakuwa unapungua kasi siku hadi siku. Tumeshaona hili kwenye nyimbo nyingi sana za wasanii wetu, ukichelewa kutoa video, wimbo unakufa haraka sana, yaani unakuwa unapungua nguvu siku hadi siku.”
-via bongo5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.