Hans Mloli, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, leo Ijumaa anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Brazil kwa ajili ya kwenda kumleta straika atakayekuja kuziba pengo la Mganda, Emmanuel Okwi klabuni hapo lakini akafunguka kuwa ada ya usajili wa Okwi imetua klabuni hapo.
Simba imefikia uamuzi huo baada ya hivi karibuni kuondokewa na Okwi aliyetua Sonderjyske ya Denmark ambapo ada ya dola 110,000 (zaidi ya Sh milioni 220) zimeshatua klabuni hapo tangu juzi.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Hans Poppe alisema fedha hizo zimeshatua na hiyo inamaana wao na Klabu ya Sonderjyske wameshamalizana rasmi.
Aliongeza kuwa anatarajia kuondoka leo saa tisa alasiri kwa usafiri wa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kupitia Uingereza halafu ataunganisha ndege nyingine itakayomfikisha Brazil ambapo atakaa huko kwa siku nne kukamilisha kila kitu.
“Nitaondoka kesho (leo). Nitatumia wiki mbili kusaka wachezaji watatu kabla ya kurejea Tanzania ambapo mbali na Brazil pia nitatembelea baadhi ya nchi za Afrika kwa ajili ya kuangalia wachezaji wengine wawili. Kwa sasa siwezi kusema ni nchi gani lakini nipe kama siku tatu au nne ndipo nitakutajia,” alisema Hans Poppe. Taarifa ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema kwamba, Simba ilikuwa na mpango wa kwenda katika nchi za Mexico na Chile kwa ajili ya kuleta wanandinga wengine lakini mpango huo wameuahirisha kutokana na kugundulika kwamba wachezaji wa nchi hizo ni ghali.

Note: Only a member of this blog may post a comment.