KWENU mastaa wawili wenye ‘taito’ ya juu
ndani ya Bongo, Wema Isaack Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond’,
mambo vipi? Mko poa?
Binafsi mimi ni mzima wa afya,
namshukuru Mungu, naendelea na majukumu yangu kama kawaida. Jukumu
nililonalo kupitia ukurasa huu ni kuwakumbuka kupitia barua hii.
Umeonesha mwanzo mzuri. Kwamba unaweza
kuwashawishi wajumbe, wakakuamini unaweza kuwatumikia, ni jambo jema.
Umethubutu kujitokeza, kweli watu wakakuona na kukupigia kura.
Wapo wengi ambao tunawajua, walijitokeza
kwa mara ya kwanza kama wewe, hawakuweza kufanikisha kura kama hizo
ulizopata wewe. Naamini una kitu cha kipekee ambacho Mungu amekupa,
usikate tamaa, songa mbele!
Nikirudi kwako Nasibu, mkali wao
uliyechipukia kutoka Tandale jijini Dar. Sina haja ya kukupongeza sana
kwa hatua ya kunyakua tuzo za MTV Africa Music (MAMA) sababu
nilishafanya hivyo wiki iliyopita. Leo nimekukumbuka tena kutokana na
tabia yako ya uswahili.
Naiita tabia ya uswahili kwa sababu ya
mambo mengi ya wivu, chuki zisizokuwa na msingi zinazofanyika sana mitaa
ya uswahilini. Majungu huko ndiko yanakopigwa na watu kupakana matope,
kukomoana na vituko vya kila aina.
Kitendo cha wewe kutupia picha ya kejeli
mtandaoni mara baada ya Wema kuonekana ameshindwa kuwania ubunge ni cha
kiswahili sana. Si cha kiungwana hata kidogo. Hakikupaswa kufanya na
mtu mwenye taito kubwa kama yako.
Eti unawashukuru wananchi wa Singida na kueleza eti mkutane Moshi kwenye shoo ya mamisi.
Nakumbuka pia hata uliposhinda tuzo za
MTV, ulimkejeli Jokate Mwegelo kwa kuweka video yake na kusindikiza na
maneno eti “mtanyooka tu.”
Jokate alilalamika. Kimsingi hukuwa pia
na sababu ya kuweka video hiyo ya zamani na kumkejeli. Huo ndio uswahili
wenyewe. Wewe hao wote walishakuwa wapenzi wako, mkaachana, acha maisha
yaendelee.
Fanya muziki wako, wape nafasi pia
wabaki kuwa mashabiki wa muziki wako hata kama penzi lilishakufa.
Usiwafanye wajute kukutana na wewe. Usiwafanye wajute kufanya kazi na
wewe.
Kwa leo inatosha, niwatakie kazi njema!
Ni mimi,
Erick Evarist

Note: Only a member of this blog may post a comment.