Friday, July 24, 2015

Anonymous

KIMENUKA MBAYA! Bodoboda Wacharuka, Nusu Wachome Moto Daladala!

Bodaboda (1)
Askari Polisi wakifika eneo la tukio.
VIJANA waendesha bodaboda walizua mtafaruku wa aina yake baada kujikusanya na kutaka kuichoma moto daladala yenye namba za usajili T 219 BSJ inayofanya safari zake kati ya Mjini na Bingwa, mkoani Morogoro ambayo ilisababisha ajali iliyomhusisha dereva bodaboda mwenzao aliyefahamika kwa jina moja la Steve.
Bodaboda (3)Bodaboda iliyogongwa na daladala ikiwa pembeni.
Tukio hilo lililozua taharuki ya aina yake miongoni mwa abiria, lilitokea juzikati maeneo ya njia panda ya Chuo Cha Ualimu cha Kigurunyembe ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Hamad Rashid ‘alimuovateki’ bodaboda kisha kusimama ghafla ndipo bodaboda alipoligonga daladala kwa nyuma.
Bodaboda (5)Polisi wakijadiliana.
“Huyu dereva wa daladala alimuovateki bodaboda sasa ghafla akaona abiria, akasimama na kusababisha bodaboda amvae kwa nyuma,” alisema shuhuda mmoja.
Bodaboda (2)Daladala iliyohusika kwenye ajari hiyo ikiwa imevunjika vioo.
Shuhuda huyo alizidi kueleza kuwa, baada ya bodaboda huyo kuligonga daladala kwa nyuma, dereva wa daladala alitimua mbio baada ya kuona vijana wa bodaboda wanakusanyika eneo hilo.
Bodaboda (6)“Dereva wa daladala alitimua mbio maana jamaa walionekana kuja kwa wingi na kuuliza dereva yuko wapi, wale vijana wa bodaboda wakawa wanatishia kuichomoa moto ndipo waungwana walipojitokeza na kuwasihi waache.
Bodaboda (7)…Wakiandika maelezo.
“Baadaye dereva wa daladala alirejea baada kuona polisi wamefika eneo hilo ambapo aliwaambia kuwa dereva huyo wa bodaboda ndiye aliyesababisha kauli ambayo haikuwa kweli,” alimalizia shuhuda huyo.
Bodaboda (8)…Wakipandisha bodaboda kwenye gari la polisi.
Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo hilo, aliwaacha askari wa usalama barabarani wakichukua maelezo kwa dereva wa daladala kwa ajili ya taratibu za kisheria huku dereva wa bodaboda ambaye alipata majeraha akipelekwa Hospitali ya Morogoro kwa ajili ya matibabu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.