Thursday, July 9, 2015

Anonymous

KEISHA Atangaza Nia, Ataka Sauti Yao Isikike Bungeni!

Msanii wa Bongo Fleva ambaye ameshawahi kuigiza kwenye filamu kadha ya kupinga mauwaji ya Albino, Keisha amefunguka kupitia ukurasa wake wa kwenye mtandao wa Instgram sababu na nia yake ya kuingia bungeni mwaka huu,na kwamba wao kama walemavu wa ngozi (Albino) lazima wawe na wawakilishi wa kutosha bungeni ili sauti zetu zisikike ili sheria itungwe na kutekelezwa pia.

Kesha ameandika;
Habari za asubuhi ndugu zangu rafiki zangu mashabiki zangu na media zote nchini.najua wengi mnajiuliza maswali mengi sana juu yangu kwanini nimeamua kuingia kwenye siasa lakini leo naomba nifunguke na kuwaambia kitu.

Mimi kama mlemavu wa ngozi najikubali najipenda na ninajiamini lakini yote tisa napigana kwa uhuru na amani ambayo tunastahili kuipata kutoka nchini kwetu.

Nilipoanza kupost picha zangu za siasa kuna ambao walinipongeza na kuna ambao walinisema kwamba sina uchungu na wenzangu kwakuwa wanahisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu.fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa nikimaanisha kwamba lazima tusimamie sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima tuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zetu zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.hivyo mimi kama mtanzania mwenzenu nahitaji support yenu ili niweze kufikia malengo yetu kwa yeyote ambaye anaupendo nasi na mimi na harakati zangu anisaidie kwa chochote ambacho kitanifikisha nnapoataka.

this is my tigo no 0718785045 na hii ni account number yangu ya crdb 011 2022295800 jina ni hadija shabani Taya unaweza kuchangia humo na kwa upendo kabisa naomba u repost hii post kadri muwezavyo ahsanteni shukrani.
Tumuunge mkono jamani.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.