Mayasa mariwata
GARI aina ya
Toyota IST lenye thamani ya shilingi milioni 13 alilotaka kulitoa bure
msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu `Bozi’ kwenda kwa msanii wa Bongo
Fleva, Ally Salumu `Ally Nipishe’ limezua utata kila kona ya jiji. Amani
linamwaga ubuyu.
“Hakuwa hivyo, Bozi nimeanza kumfuatilia kipindi kirefu na huwa namuona mara kwa mara akitumia usafiri wetu wa daladala siku nyingine Bajaj, sasa ana jeuri gani mjini ya kumnunulia gari mwanaume?” alihoji Juma Mongolla mkazi wa Tabata.
Amani lilimtafuta Bozi ili kusikia kauli yake kuhusu gari hilo ambapo alifunguka;
“Mimi ni mtoto wa kike siwezi kufa njaa hapa mjini, maisha yangu kwa sasa ni mazuri kwani nina mwanaume mwenye pesa anayeniwezesha katika biashara zangu.
“Sifahamiani kabisa na Ally ila nikiwa kama shabiki wake katika muziki, niliguswa na matatizo yaliyompata ndiyo maana nikaona nimpe zawadi ya gari,” alisema Bozi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.