Thursday, July 23, 2015

Anonymous

CHADEMA Waliteka Mwanza? Kambi ya LOWASSA na MAGUFULI?! Dar BVR Zimeanzaje? Hali ya Burundi baada ya Uchaguzi ikoje? (Audio)

recording_sound_board
Hapa ninao uchambuzi wa story kubwakubwa za Magazetini July 23 2015, nimekusogezea kwenye maandishi na unaweza kusikiliza pia sauti mtu wangu. 

CHADEMA waiteka Mwanza kwa saa sita, Freeman Mbowe aahidi CHADEMA kuleta kiongozi atakayekubalika na nchi nzima… kuna stori kuhusu uandikishaji kwa mfumo wa BVR Dar es Salaam kuanza vibaya jana kutokana na upungufu wa vifaa, uwezo mdogo wa wafanyakazi, upungufu wa watendaji na ukosefu wa umeme. 

Kutoka Morogoro iko stori inayohusu Mahakama ya Hakimu Mkazi kumfutkia shitaka moja Sheikh Ponda, kwa sasa atatakiwa kujibu mashitaka mawili… Stori nyingine kubwa inahusu Prof. Anna Tibaijuka kushushwa jukwani kwa kuzomewa alipokuwa akihutubia Muleba, baadhi ya makada wa CCM waliokuwa kwenye kambi ya Urais ya Lowassa wakutana na Dk. Magufuli faragha. 

Iko nyingine kubwa kutoka Burundi, hali sio shwari kwa sasa licha ya Uchaguzi wa kumpata Rais wa nchi kufanyika siku ya Jumatatu wiki hii.
Hizo zote ziko na kwenye sauti hapa, ukiplay utazipata zote mtu wangu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.