Kwenye mfululizo wa matukio yaliyoshtua
watu wengi Tanzania, liko pia ambalo lilitokea usiku wa July 12 2015
ambapo Majambazi walivamia Kituo cha Polisi Stakishari Ukonga Dar, wakauawa watu 7 wakiwemo pia Askari wanne na watu wengine watatu.
Leo taarifa imetolewa na Kamanda Suleiman Kova
kwamba kuna watu watano wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo na pia
kuna silaha ambazo zimekamatwa, ziko Bunduki 15 pamoja na Risasi 28
ambazo zote ni sehemu ya zilizoibiwa wakati wa tukio la Ujambazi
uliofanyika Stakishari.
Note: Only a member of this blog may post a comment.